Ewald Frank

Kwa Kanisa Bibi-arusi la Yesu Kristo

Natamani kutuma salamu za kujaa moyo kwa wandugu na wadada wote ulimwenguni kote ambao wameamini wa ujumbe safi ya kibiblia wa Mungu na sasa wanaishi mazoefu ya matayarisho yao ya Unyakuo, kwa Neno la BWANA kutoka kwa Isaya 55:11: “Ndivyo litakavyokuwa neno langu litokalo katika kinywa changu, halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.”

Maandiko yafuatayo ya kibiblia yamekusudiwa kutuonyesha kile ambacho Bwana Mungu anatarajia kutoka kwetu, ili kile tunachotarajia kutoka kwake na kile anachotaka kutupatiya kwa neema kiweze kutimizwa, kwa lengo la kuwa tuko tayari wakati atakapo rudi.

Kurudi kwa Kristo kumekuwa tumaini la waamini wote wa kweli tangu mwanzo. Katika Yohana 14:2-3 Bwana wetu alisema,  “Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia. Naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.”

Katika Maandiko Matakatifu, Ujio wa Pili wa Kristo unasisitizwa tena na tena: “Kazalika Kristo naye ,akiisha kutolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi; atatokewa mara ya pili, pasipo dhambi, kwahao wamutazamiao kwa wokovu.” (Waebrania 9:28). Imeandikwa tayari kuhusu Henoko: “Kwa imani Henoko alihamishwa, asije akaona mauti; wala hakuonekana, kwa sababu Mungu alimhamisha; maana kabla ya kuhamishwa alikuwaameshuhudiwa kwamba amempendeza Mungu. (Waebrania 11:5)

Bwana pia alizungumza juu ya mambo yote yatakayotokea katika nyakati za mwisho kabla ya Kurudi kwa Kristo, iwe inahusu Israeli, Kanisa, au hali ya jumla duniani:

„Hata alipokuwa ameketi katika mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamwendea kwa faragha, wakisema, Tuambie, mambo hayo yatakuwa lini? nayo ni nini dalili ya kuja kwako, na ya mwisho wa dunia? “

Yesu akawajibu, “…Agalieni mtu asiwadanganye…” Alizungumza kuhusu vita, njaa, matetemeko , magonjwa ya kuambukiza, na mengineo (Mat 24:3-7) na alisisitiza hasa, “Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.” (Mt 24:14) Leo Maandiko haya yanatimizwa mbele ya macho yetu katika ulimwenguni pote.

Katika Luka 21:28 Bwana aliwaambia walio Wake kuhusu matukio ya nyakati za mwisho: “Basi mambo hayo yaanzapo kutokea, changamkeni, mkaviinue vichwa vyenu; kwa kuwa ukombozi wenu umekaribia.”

Kabla ya Kurudi Kwake, hata hivyo, kila kitu lazima kirejeshwe kwa nafasi yake katika Kanisa, jinsi ilivyokuwa hapo mwanzo, kama vile Matendo 3:21 pia inavyosema: “Ambaye ilimpasa kupokewa mbinguni hata zije zamani za kufanywa upya vitu vyote, zilizonenwa na Mungu kwa kinywa cha manabii wake watakatifu tokea mwanzo wa Ulimwengu”.

Hii ni pamoja na ahadi kwamba mwishoni mwa wakati wa neema, kabla ya siku ya kutisha ya Bwana haijapambazuka, Mungu angetuma nabii ambaye angegeuza mioyo ya watoto wa Mungu irudi kwa baba zayo mitume. Ahadi hii ya Malaki 4:5-6 imetimizwa kupitia huduma ya Ndugu Branham. Kuhusu tukio la Unyakuo wenyewe, tunasoma katika 1 Wathesalonike 4:15-17: “Kwa kuwa twa waambiani haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliyokwisha kulala mauti. Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; Nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai,na tuliosalia, tutanyakuliwa pamojanao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.”

Wafilipi 3:20-21 inasema: “Kwa maana sisi wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo, atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake.”

Sharti la hili ni kwamba Neno lifuatalo litimie ndani yetu: “Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu.” (Warumi 8:11)

Ahadi hii itakuwa ukweli wenye uzoefu wakati wa Kurudi kwa Bwana wetu.

Wakati huo huo, tunaonywa kusimama imara na kumngojea Mungu akamilishe kazi Yake kwa nguvu ya kitendo cha Roho Mtakatifu: “Kwa hiyo ndugu, vumilieni, hata kuja kwake Bwana. Tazama, mkulima hungoja mazao ya nchi yaliyo ya thamani, huvumilia kwa ajili yake, hata yatakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho. Nanyi vumilieni; mthibitishe mioyo yenu, kwa maana kuja kwake Bwana kunakaribia.” (Yak 5:7-8)

„Furahini, basi, enyi wana wa Sayuni, mkafurahie Bwana, Mungu wenu; kwa kuwa yeye huwapa ninyi mvua ya masika kwa kipimo cha haki, naye huwanyeshea mvua, mvua ya masika, na mvua ya vuli kama kwanza.” (Yoeli 2:23)

Kwa kuwa hakuna ajuaye saa kamili ya Kurudi Kwake, tunahimizwa kuwa tayari kila wakati: “Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa maana katika saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja.” (Mt 24:44)

Ni lazima pia tuchukue Neno hili zito kwa moyo wetu: “Basi, ikiwa igaliko ahadi ya kuingia katika raha yake, Natuogope, mmoja wenu asije akaonekana ameikosa. Maana nikweli, sisi nasi tumehumbiriwa habari njema vile vile kama wao; lakini neno lilelilosikiwa halikuwafaa hao, kwasa babu halikuchanganyika na imani ndani yao waliosikia.” (Waebrania 4:1-2) Ibrahimu alimwamini Mungu na aliona ahadi ikitimizwa, nasi tunamwamini vivyo hivyo Mungu na Neno Lake nasi tutaona utimilifu wa ahadi.

Kama Paulo, ambaye alichukua huduma yake kwa Bwana kwa uzito, ningependa pia kuwahimiza waamini wote kusoma kwa uangalifu Maandiko yafuatayo: “Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.” (Warumi 12:1-2)

„Apate kuifanya imara mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu, Baba yetu, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo pamoja na watakatifu wake wote.” (1 Wathesalonike 3:13)

„Mukishika neno la uzima; nipate sababu ya kuona fahari katika siku ya Kristo, yakuwa sikupiga mbio bure, wala sikujitaabisha bure. (Wafilipi 2:16)

„Na hii ndiyo duwa yangu, kwamba pendo lenu lizidi kuwa jingi sana ,katika hekima na ufahamu wote; Mpate kuyakubali yaliyo mema; ili mpate kuwa na moyo safi, bila kosa mpaka siku ya kristo; hali mumejazwa matunda ya haki, kwa njia ya Yesu Kristo, kwa utukufu na sifa ya Mungu.” (Wafilipi 1:9-11)

Nia yetu ya kilindi ni kwamba Maandiko haya yote ya kibiblia yatimie, ndani yetu na kupitia sisi.

„Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.” (1 Wathesalonike 5:23)

„Na sasa, watoto wadogo, kaeni ndani yake; ili kusundi,atakapo funuliwa muwe na ujasiri, wala musiaibike mbele zake katika kuja kwake. (1 Yohana 2:28)

„Maana tumaini letu, ao furaha yetu, ao taji yakuoneafuhari ni nini? Je! si ninyi mbele za Bwana wetu Yesu, wakati wa kuja kwake?” (1 Wathesalonike 2:19)

Hii inarejelea wale wote ambao Mungu amewachagua kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. Ni kwa hao ambao Mtume anaambiya maneno haya mazito: “Wala msimhuzunishe Yule Roho Mtakatifu wa Mungu, ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi.” (Waefeso 4:30)

Ni wale tu wanao fanya sehemu ya Kanisa Bibi-arusi ndio watakao wekwa muhuri, nani kwawao maonyo haya yamuhimu ya kutomhuzunisha Roho wa Mungu kwa kutokuamini na kutotii. Lakini nina amini kwamba maneno yale ambayo Mtume aliwaandikia wandugu na wadada kwa wakati wake bado yanatuhusu sisi leo: “Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu…” (Wafilipi 1:6)

Ndugu Branham alitimiza hudma yake ya kibiblia na kuleta ujumbe unaotangulia Ujio wa Pili wa Kristo. Nilitumiwa na Bwana kubeba ujumbe wa mwisho, Neno lililofunuliwa, katika ulimwengu wote baada ya kupita kwake. Ndugu wote wahudumu wa kweli huhubiri Neno lile lile na kushiriki ungawaji wa chakula kile kile cha kiroho, na hivyo Kanisa Bibi-arusi linaletwa katika umoja wa Roho nakwa hatuwa moja na Neno.

„Na hao walipokuwa wakienda kununua, bwana arusi akaja; nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini, na mlango ukafungwa.” (Mt 25:10)

„Tazama, naja upesi!“

„Na Roho na Bibi-arusi wasema, Njoo!“ (Ufu 22:17)

Kwa mwaka wa 2023, tunatazamia Mungu afanye mambo makuu na kutimiza ahadi zake pamoja kwa kila mmoja wetu. Tunaweza kuwa na uhakika kwamba Neno Lake litatimiza yale ambayo lilitumwa kufanya kwa wote wanaoliamini, na kutimiza ile aliyoahidi. Amina!

Kwa agizo lake

Ewald Frank